GIGY MONEY ATAJA DAU LA ”PAPA” KWA YEYOTE ANAEMUHITAJI.

Msanii wa Bongo Fleva na Video vixen, Gigy Money amesema kwa sasa kama promota au mtu yeyote anayehitaji kumuita kutumbuiza kwenye tamasha/sherehe yake basi ni lazima uwe na kiasi cha milioni mbili za kitanzania.

Mkali huyo anayetamba kwa sasa na wimbo wake wa ‘Papa’ amesema wimbo huo ni ‘Hit Song’ na ni moja ya wimbo mkali kwa sasa kuliko nyimbo nyingine zilizotoka kwa muda huu. “Na-perform stejini kwa milioni mbili, Papa is a hit song, bila milioni 2 siwezi kutoa Papa stejini, is a hit song.“amesema Gigy Money kwenye mahojiano yake na moja ya chombo cha habari za burudani. Pia amesisitiza Papa ni Hitsong kuliko Seduce me

Ya Ali Kiba watu wanatakiwa kukubali.