FLAVIANA MATATA KUWAIMBISHA KISERA NA SEDUCE ME, SWIZZ BEAT NA FABILOUS. DIAMOND PLATNUMZ NA MWANA FA, WASALIMIWA.

Producer mkongwe wa muziki nchini Marekani, Swizz Beatz ameingia rasmi kwenye fashion na jana kwa kushirikiana na kampuni ya Switzerland, Bally na msanii wa Hispania, Ricardo Cavolo amezindua nguo, viatu, mabegi, kava za simu, sandals, majaketi za bidhaa zingine kibao.
Uzinduzi huo ulihudhuria na mastaa kibao akiwemo Flaviana Matata na hapo ndipo palikuwa patamu. Flavy amepost video za event hiyo ambao miongoni mwa nyimbo zilizochezwa ni pamoja na Seduce Me ya Ali kiba… Na Kisela ya Vanessa Mdee. baada ya hapo Flavy alisalimiana na mke wa Swizzz Beat, Alicia Keys, akakutana na man of the night, Swizz ambaye alituma salama kwa Watanzania na specifically, Diam ond Platnumz.
Kisha, Flavy akakutana na rapper Fabolous ambaye akamuambia kuwa ana pacha wake Tanzania ambaye ni MwanaFA. Flavy pia alipiga story na muimbaji nguli wa rnb soul Maxwell.
Flavy amekutana na mastaa hao A LIST wa Marekani, wiki moja tu baada ya kukutana na Beyonce na Jay Z na kusalimiana nao kama anavyokutana tu na staa wa Bongo. Mrembo huyo anafanya kazi kubwa kuitangaza Tanzania, anastahili pongezi kubwa.