DIWANI WA CHADEMA KATA YA AMBULEN AJIUZULU LEO TAREHE 12.07.2017

Salamu Sana:

Napenda Kutoa Taarifa Kwa Umma Wa Wananchi Wa Kata Ya Ambulen Kuwa Diwani Wa Chadema Ndugu Japhet Joseph Jackson Amejiuzulu Leo Ili Apate Nafasi Nzuri Ya Kumuunga Mkono Rais John Pombe Magufuli Kwa Kazi Nzuri Anayofanya Kuwatumikia Wananchi Wa Taifa Hili.

Mh. Japhet Jackson Anakuwa Diwani Wa Sita Hapa Wilayani Arumeru Kujiuzulu Kwenye Nyadhifa Hiyo kwa Kazi Nzuri Zinazofanywa Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Hususani Uchapakazi Wa DC Mnyeti Katika Wilaya Anayoishi Kwani Amekuwa Chachu Ya Maendeleo Kwa Wananchi Wa Arumeru.

Mosi Diwani Ndugu Japhet Joseph Jackson Anakiri Wazi Kuwa Kabla Ya Kuchukua Uamuzi Huo Mgumu Na Sahihi Wa Kujiuzulu Alikuwa Kwenye Mfungo Wa Wa Maombi Wa Takribani Siku Arobaini (40) Ili Mwenyezi Mungu Amsaidie Katika Maamuzi Hayo, Mintarafu Diwani Anasema Wazi Kwamba Maslahi Mapana Ya Wananchi Ni Zaidi Kuliko Chama Kwani Pamekuwa Na Mgogoro Usiokwisha Wa Madiwani Wenzake Wa Chadema Kupinga Kila Jambo Zuri linalofanywa Na Mkuu Wa Wilaya Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yake Kuwatumikia Wananchi Pasipo Upendeleo Wa Kiitikadi.

Aghalabu Diwani Japhet Joseph Jackson Anaendelea Kutoa Shukrani Za Dhati Kwa Mh. Rais John Pombe Magufuli Kwa Zuio Lake La Usafirishaji Na Uuzaji Wa Udongo Wa Dhahabu Ambapo Kulingana Na Maandiko Ya Mishahafu Kama Biblia Inasema Wazi Anayeuza Udongo Anauza Baraka Na Urithi Wa Nchi Yake Hivyo Atalisimamia Hilo Mpaka Mwisho Kwa Kuungana Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Kwa Kumuombea Rais Magufuli Kwa Mungu.

Diwani Japhet Anahitimisha Kwa Kutoa Pongezi Za Dhati Sana Kwa Mkuu Wa Wilaya DC Mnyeti Na Kwa Serikali Ya Awamu Ya Tano Chini Ya Rais John Pombe Magufuli Kwa Uchapakazi Wao Katika Utendaji Uliotukuka Kwa Kumweka Mungu Mbele Kuhakikisha Nchi Inapata Maendeleo Makubwa Hususani Katika Kata Yake Ya Ambulen Na Ametoa Nasaha Kwa Wananchi Kuunga Na Serikali Ya Wilaya Kwa Kumuunga Mkono Rais Na Mkuu Wa Wilaya Bwana Mnyeti.

Diwani Japhet Joseph Jackson Amekabidhi Barua Zake Zote Kwa Maandishi Kwa Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Meru Na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya Kama Kumbukumbu Sahihi Ya Kujiuzulu Kwake Leo Tarehe 12.07.2017

Wasalamu.

Na Mwandishi.;Titho Cholobi.