CUF YAMUONYA MBOWE KUACHA KUMKASHIFU PROF. LIPUMBA KATIKA MIKUTANO YAKE

Chama cha Wananchi (CUF),kimeeleza kusikitishwa kwake na kauli za maudhi na zenye kuleta chokochoko zilizotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Nd. Freeman Mbowe huko Mtwara.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma (CUF), Abdul Kambaya inaeleza kuwa, kauli zinazotolewa na Mbowe zinayoonyesha kuwa, Chama hicho kimekosa agenda kwenye Chaguzi ndogo zinazorejewa kwenye Kata 43.

Aidha, taarifa hiyo imefafanua kuwa, hii inaonyesha wazi kuwa, Chadema imeamua kuanzisha mashambulizi yasiokua na tija kwa Wapiga Kura wa Kata husika na wala kwa Chadema yenyewe kama Chama ambapo imeacha kueleza Sera za Chama chao kwa wapiga Kura ili iwe chachu ya kuchaguliwa kwa Wagombea wao, lakini Freeman amegeuza majukwaa hayo kuwa uwanja wa mashambulizi binafsi dhidi ya Profesa Lipumba.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa, CUF-Chama cha Wanachi sio tu wameshangazwa lakini pia wanajiuliza kwani Prof Ibrahim Lipumba ni mgombea wa Kata ipi kati ya hizo zinazorejea Uchaguzi?

“Hivi Mbowe anaweza kuhoji Uprofesa wa Lipumba kwani hajui sehemu za kupata majibu yake?, kama hajui basi tunamsaidia na aende UDSM au William College Marekani atapata majibu ya swali lake kama yeye hawezi kufika maeneo hayo basi watafute wenye kuweza kufika maeneo hayo”, ilihoji taarifa hiyo.

Ilifafanua kuwa, CUF haina cha kuhoji wala kuuliza Mbowe ni Mwenyekiti wa aina gani kwakua kinamtambua vyema na hasa kupitia wakati wa uhai wa Club Bilcanas kwa hivyo mtazamo na fikra hasi sio tu dhidi ya Prof Lipumba lakini pia hata kwa Siasa za Nchi yetu ni matunda ya Club Bilcanas.

Pia imeeleza kuwa, Mhe Mbowe anafahamu kwamba yeye na Prof Lipumba ni sawa na mlima Kilimanjaro na kichuguu kuhusu elimu hivyo kuhoji elimu ya Prof Lipumba ni kichekesho sana.

Mhe Mbowe anatambua sababu ya Prof Lipumba na Dkt Slaa kutoshiriki Kampeni za kumnadi Lowassa ni kutokana na Mgombea huyo kukosa sifa za Uadilifu na tuhuma mbalimbali za Ufisadi zilizoelezwa hata na yeye mwenyewe Mbowe.

Ilifafanua kuwa, Mbowe sio mkweli hapo Mtwara mjini licha ya kuwepo kwa mashirikiano ya UKAWA chadema iliweka mgombea na mgombea na alishinda wagombea wote wa CDM,CCM,ACT-WAZALENDO,na NCCR-MAGEUZI, lakini katika hotuba yake amedai kuwa, Mtwara mjini hawakuweka mgombea.

Taarifa hiyo ilimalizia kuwa, siasa za Utapeli zimepitwa na wakati ni vema tukajikita kueleza kero za watu na namna ya kuzitatua na wanamfahamisha Mbowe na wenzake kwamba, CUF hawahitaji chokochoko na kwamba kuanzia sasa kitendo chochote cha kumkashifu Mwenyekiti wetu hakitavumilika.

Ikamaliziankuwa, watajibu kwa mifano hai itayoleta tija kwa Jamii kwani kila jambo litavuliwa nguo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*