CUF YA MAALIM YAWAPONGEZA WABUNGE WA UPINZANI NA KUTOWATAMBUA WABUNGE WALIOTEULIWA.

Chama cha Wananchi (CUF) upande unaomuunga mkono Maalim Seif kimewapongeza wabunge wote wa kambi ya upinzani Bungeni kwa kuonyesha umoja na kuweka msimamo wa pamoja kwa kutoshirikiana na wanachama wote wanaodhaniwa kuenda kinyume na matakwa ya chama hicho.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Bunge kuwaapisha jana wabunge saba wanaomuunga mkono Professor Ibrahim Lipumba, pamoja na hatua hiyo Baraza kuu la Uongozi la taifa wakiongozwa na Maalim Seif wamesisitiza kuendelea kuwatambua wabunge walioteuliwa na baraza kuu hapo awali na kudai kua msimamo huo hautabadilika na kuongeza kua wanaendelea na msimamo wao wa kuwatambua Wabunge na Madiwani waliodaiwa kuvuliwa uanachama kua bado ni wanachama halali wa CUF.

Aidha, chama hicho kimetoa wito kwa wanachama na viongozi wote nchini kutowapa ushirikiano wowote ule na kutowatambua wabunge walioteuliwa kwa nafasi hizo za ubunge na kudai kua ni nafasi feki walizopewa kwa lengo la kuihujum taasisi ya CUF.

Hata hivyo upande huo wa chama cha CUF kimewatoa hofu wanaCUF kwa ujumla na kueleza kua masuala haya bado yanaendelea Mahakamani na wana imani kubwa na mahakama kuwa itasimamia na kutenda Haki.