CONTE: CHELSEA HILI HAPA NDIO TATIZO.

Msimu huu wa ligi ya Epl mabingwa watetezi Chelsea wanaonekana kuhangaika kupata matokeo na mbaya ni kwamba hadi sasa wamefungwa na timu ambazo hakuna aliyetaraji zingewafunga.

Walifungwa na Burnley mwanzoni mwa msimu na kisha wakapigwa na Man City, sasa Crystal Palace nao wamewafunga siku ya jana ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo jambo ambalo hakuna mfuatilia soka ambaye angedhani lingetokea kirahisi.

Lakini baada ya mchezo huo kuisha kocha wa Chelsea Antonio Conte amekiri kwamba timu yake inakosa balance na ndio maana hata katika mchezo wao dhidi ya Crystal Palace haikuwa rahisi wao kupata matokeo.

Conte anasema kama timu isipokuwa na balance ni ngumu kucheza vizuri lakini akasisitiza kwamba kukosekana kwa kiungo wao mkabaji Ngolo Kante kunawafanya wakose balance katika timu yao.

Ilibidi Conte amchezeshe Tiemoue Bakayoko na Cesc Fabregas katika eneo la kiungo wa kati jambo ambalo ndilo lililowafanya kukosa uwiano mzuri uwanjani kwani Kante alikuwa anacover uwanja mzima tofauti na Cesc ambaye ni mzuri akiwa na mpira.

Ngolo Kante anatariji kukaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja na wiki mbili, mara ya mwisho kwao kupoteza mechi mbili mfululizo ilikuwa 2016 huku kipigo cha Chelsea cha jana kimewafanya kukaa katika nafasi ya 5 wakiwa na alama zao 13.