CHADEMA IRINGA YAMEGUKA,MADIWANI WATATU WAACHIA NGAZI

Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Manispaa ya Iringa kimepata pigo baada ya madiwani watatu kujivua uwanachama na udiwani kutokana na changamoto zilizopo kwenye chama hicho.

Tukio hili limetokeo leo wakati wa Katibu mkuu wa chama hicho Vincent mashinji akiwa ziarani mkoani Iringa kwa ajili ya kuimalisha na kukijenga chama kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuongea wanachama na utendaji wa madiwani na wabunge wa hao.

Wakizungumza na waandishi wa habari madiwani hao ambao ni Leah mleleu,Baraka kimata na Husna Daudi walisema kuwa wameamua kuchukua jukumu hilo zito kutokana na udikteta unaofanywa na viongozi wa chama hicho hapa Manispaa ya Iringa.

Kimata alisema kuwa madiwani wa chama cha CHADEMA Manispaa ya Iringa wamekuwa wakimnyeyekea mbunge.

Kikubwa kilichosemwa na madiwani wote ni uongozi wa kidikteta unaoendelea ndani ya chama hicho na huku viongozi wa juu wa chama hicho wakiwa kimya