CCM IKO TAYARI KUKOSOLEWA NA KUSAHIHISHWA

Na Fahamu Mastawili

Moja ya Democrasia kubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ni Uhuru wa Mawazo kwa kila Mwanachama wake ukilinganisha na Uhuru wa Mawazo ndani ya Vyama Vingine Maana Utofauti wa Mawazo ndio Afya ya Taasisi yoyote Duniani lakini ni Muhimu Utofauti ya mawazo hayo iwe ni ya kujenga,Kuboresha, au kwenda mbele zaidi kwa Taasisi au Taifa husika (Constructive idea).

Wabunge wetu kwa Mujibu wa Katiba yetu ya 1977 ya ibara ya 63 (2.3) ni chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kuishauri na kuisimamia serikali lakini hili liwe na tija lazima wabunge wetu wawe informed with researched report, ili Kuisimamia na kuishauri serikali Vizuri kwa maslahi ya Taifa letu.

Jana nimemsikia kaka yangu Nape Nnauye Bungeni akipinga na kutoa tahadhari kwa kitendo cha serikali kuamua kutumia fedha za Wananchi kujenga miradi mikubwa.

Kwa maelezo kuwa ni hatari kwa Uchumi wa Nchi na ni makosa makubwa yamefanywa serikali itakosa fedha za kupeleka huduma za kijamii kwa Wananchi na badala yake miradi hiyo mikubwa ingejengwa na sekta Binafsi sio serikali.

Kaka Nape Nnauye nakuomba usome Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2015/2016.

Ripoti ya CAG inaonesha Shirika la Umeme Tanesco linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 863.48 deni kutoka kwa makampuni mbali mbali yanayozalisha Umeme kama Independent Power Tanzania Limited (IPTL), SIMBION POWER, AGGREKO.

Ripoti ya CAG inaonesha Shirika la Tanesco linanunua Umeme Unit Moja kwa Shilingi 544.65 kutoka kwa Makampuni haya yanayozalisha Umeme na Kuuza Umeme huo kwa Wananchi Unit moja kwa Shilingi 265.30 hali inayosababisha shirika kujiendesha kwa Hasara.

Ushauri wa CAG kwenye ripoti nanukuu, “Ofisi ya CAG inaishauri Serikali kumalizia Mradi Maji ya Korongo la Stiegler Gorge ambao ulikuwa unasimamaiwa na mamlaka ya Bonde la Rufiji (Rubada) Mradi Ukimalizika Utaweza kuzalisha Megawati 2100 za Umeme” mwisho wa kunukuu.

CAG amepewa mamlaka ya kufuatilia kila shilingi ya inayotumiwa na serikali kwa mujibu wa katiba yetu ibara ya 143.

Ushauri wa Nape Nnauye kuhusu kupinga serikali kujenga Miradi mikubwa kwa kutumia fedha zake Mapungufu mengi moja wapo ni.

1. Jukumu la serikali kwenye Uchumi wa Soko ni kutengeneza mazingira rafiki (A conducive environment) kujenga Miundombinu (barabara, Umeme, Mawasiliano ya Anga, Majini, ya mtandao, Reli.)

Ili kuvutia uwekezaji kwa Sekta binafsi na sekta Binafsi inaweza kuendesha miradi ya uzalishaji au Utoaji huduma kwa njia ya leseni kutoka kwa serikali lakini lakini ukiruhusu sekta binafsi ijenge miradi mikubwa inawezekana kabisa mwananchi wa kawaida atabeba gharama kubwa katika kupata huduma ya miradi hiyo itakapoanza kutumika.

2. Miradi yote hii ni Muendelezo kutoka serikali za nyuma ila serikali ya Awamu ya Tano imeamua kufanya Maamuzi magumu katika utekelezaji wa project za Miradi hii mikubwa kama mradi wa Umeme wa Stiegler Gorge kutoka serikali ya Awamu ya kwanza na mradi wa ujenzi wa reli.. inawezekana ilishindikana kutokana na Uhaba wa fedha au Utashi wa kisiasa.

Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kujenga Reli ya standard gauge ambayo Ubora wake na kiwango chake Afrika mashariki Mashariki hakuna..Kenya Wamejenga Reli ya standard gauge kutoka Nairobi hadi Mombasa kwa fedha za mkopo na hakuna nchi yoyote Duniani imeendelea kiuchumi bila kuwa na Usafiri wa Treni.

Mwananchi wa Kagera Bukoba badala ya kusafirisha mizigo siku 3 njiani kutoka Dar es salaam hadi Bukoba sasa Mradi wa Reli Ukimalizika mwananchi wa kagera Bukoba ataweza kusafirisha mizigo yake kutoka Dar es salaam hadi Bukoba au Bukoba hadi Dar es salaam kwa Siku moja na Nusu na kwa Gharama nafuu sana kuliko ilivyo hivi sasa usafiri wa magari.

Mfano ndizi Bukoba na Maharage zitapakiwa kwenye Meli Usiku na asubuhi yake Mapema Ndizi zitakuwa Mwanza zatapakiwa kwenye Treni ya kisasa saa saba mchana ndizi na Maharage yatakuwa Dar es salaam sokoni.

Uchumi wa Wananchi Utakuwa Vizuri na hiyo ndio kazi ya serikali kujenga Miundombinu ili sekta binafsi ipate Urahisi katika utoaji huduma na Uzalishaji na serikali ipate kodi yake.

3. Sekta Binafsi haiwezi kuwekeza kwenye project yoyote hadi iwe na uhakika wa security and Value for money miradi gharama ya Ujenzi wa reli ya standard karibu Trilioni 17 zinarudije lazima gharama ya usafirishaji mizigo na Abiria gharama iwe juu kuliko malengo ya serikali kuanzisha Miradi mikubwa kuwasaidia wananchi wetu………

4. Baada ya nchi yetu kuhama kutoka kwenye mfumo wa Uchumi Hodhi ambao serikali ilikuwa Inazalisha na kutoa huduma kwa wananchi ikahamia kwenye uchumi wa soko lakini pamoja na Kuwa kwenye Uchumi wa soko serikali iliendelea kutoa huduma kwa wananchi katika mfumo wa Cost sharing mfumo ambao mwananchi anachangia kidogo na serikali inachangia kidogo katika kutoa huduma za kijamii mfano Afya, Maji, Umeme, Elimu n.k

Mfumo wa Cost sharing ulilenga serikali na mwananchi kusaidiana katika kugharamia gharama za huduma ili mwananchi asibebe mzigo wa gharama kubwa ya kupata huduma mfano Umeme Tanesco inanunua unit moja ya Umeme kwa shilingi 544.65 kutoka kwa Makampuni haya yanayozalisha Umeme na Kuuza Umeme huo kwa Wananchi Unit moja kwa Shilingi 265.30 hali inayosababisha shirika kujiendesha kwa Hasara.

ina maana kama serikali ingeacha IPTL,SIMBION POWER, AGGREKO ndio waende moja kwa moja kuuza Umeme kwa Wananchi ina maana mwananchi angeuziwa kwa shilingi 544.65 kwa Unit moja

Hivyo mwananchi aliyekuwa ananunua Umeme wa shilingi 10,000 anapata Unit 28 kwa gharama ya shilingi 265.30 kwa unit moja sasa umeme wa shilingi 10,000 zitakuwa Unit 18 kwa gharama ya shilingi 544.65 kwa Unit moja..

Abiria wa Treni daraja la chini kutoka Dar es salaam hadi Tabora analipia shilingi 26,000 ina maana ili sekta binafsi waweze kurudisha fedha zao wakiwekeza kwenye mradi mkubwa wa standard gauge lazima nauli zipande zaidi lazima gharama za usafirishaji wa mizigo ipande zaidi kuliko mategemeo ya wananchi kwenye miradi mikubwa hii ikikamilika kusafirisha mizigo yao kwa gharama nafuu na Nauli itakuwa nafuu kuliko usafiri wowote.

Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana Tuwe na Mawazo Sahihi na ya Kujenga.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*