HAT TRICK YA MESSI YAIPELEKA ARGENTINA URUSI KOMBE LA DUNIA 2018

Usiku wa kuamkia leo umekua usiku wa kipekee kwa wapenzi wa soka wa argentina na duniani baada ya kuishuhudia timu hiuo ikifuzu kimiujiza kombe la dunia 2018.

Argentina ilikua katika hatihati ya kutokushiriki fainali hizo na ilitakiwa kushinda mchezo wa leo dhidi ya Ecuador ambapo mshambuliaji tegemeo na nahodha wa timu hiyo Leonel Messi alifanikiwa kulibeba taifa hilo kwa kupachika mabao matatu hatatrick katika mchezo huo.

Magoli ya Messi yaliwekwa kimiani dakika za 11, 18 na 62 ambapo licha ya ecuador kutawala mchezo huo lakini maajabu ya Messi yalitosha kubadili upepo na hivyo kufuzu fainali hizo.

Argentina inaungana na mataifa mengine ya Amerika ya kusini kama Brasil, uruguay na Colombia kushiriki fainali hizo nchini urusi mapema mwakani.