ATANGAZA ZAWADI YA DOLA MILLIONI 10 KWA ATAKAYEFANIKISHA KUMNG’OA TRUMP.

Larry Flynt ambaye ni mmiliki wa jarida maarufu la picha za utupu la Hustler  amechapisha tangazo katika gazeti la Washington Post, akiahidi kulipa zawadi ya dola milioni 10, kwa mtu mwenye habari, zitazopelekea Rais Trump kushtakiwa na kuondoshwa madarakani. 


 Flynt, amesema ni wajibu wa kila Mmarekani, kumuondoa Rais Donald Trump, kabla ya kuchelewa kwani matendo yake yanachafua taswira ya taifa la marekani. 

Katika tangazo hilo, ametoa nambari ya simu ya kupiga na anuani ya barua pepe kwa yeyote atayefanikisha takwa hilo.

Larry Flynt, ambaye alikuwa mfuasi mkubwa wa Hillary Clinton katika kuwania urais, ametoa matangazo kama hayo kabla, lakini hakuwahi kutoa zawadi kubwa kama hiyo.