ACT Wagoma Kupekuliwa, Polisi Wamfuata Katibu Mkuu Nyumbani

Updates: ACT Wagoma kupekuliwa, Polisi wamfuata Katibu Mkuu nyumbani

Askari wa Jeshi la Polisi, wamefika Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo na kukutana na Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mawasiliano ya Umma, ndugu Ado Shaibu, ambaye baada ya kuwapokea amewaeleza kuwa mwenye Ofisi ni Katibu Mkuu ambaye hayuko Ofisini, na kuwa kama Jeshi la Polisi lilitaka kufanya Upekuzi kwenye Ofisi za ACT Wazalendo, nafasi nzuri kwao ilikuwa ni jana kwa kuwa walimhoji Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwa Masaa 7.

Polisi wamesisitiza kufanya upekuzi leo, hivyo wameamua kumfuata Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, nyumbani kwake ili awepo wakati wa upekuzi husika.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*