ACT Wagoma kupekuliwa • Polisi wamfuata Katibu Mkuu nyumbani

darmpya#Updates:ACT wagoma kupekuliwa.
. Polisi wamfuata Katibu Mkuu nyumbani kwake

Askari wa Jeshi la Polisi wamefika katika ofisi za Makao Makuu ya ACT na kukutana na Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Ndg. Ado Shaibu, ambaye baada ya kuwapokea askari hao aliwaeleza kuwa, mwenye ofisi ni Katibu Mkuu ambaye kwa wakati huo hakuwepo ofisini na kwamba Jeshi la Polisi lilihitaji kufanya upekuzi kwenye ofisi za ACT Wazalendo, walikuwa na nafasi nzuri hapo jana kwa kuwa walimhoji Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwa masaa saba.
Hata hivyo pamoja na askari kupewa maelezo hayo, walisisitiza kufanya upekuzi huo leo Novemba 7, na hivyo kuamua kumfuata Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Ndg. Dorothy Semu, nyumbani kwake ili awepo wakati wakifanya upekuzi huo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*