TANZANIA YAFANYA VIZURI KATIKA UTOAJI MIKOPO-TPSF

Na John Marwa
Tanzania yafanya vizuri kwa baadhi ya vipengele, licha ya kuwa imeporomoka kwa nafasi tano katika ripoti ya Benki ya dunia ya urahisi wa kufanya biashara Duniani ukilinganisha na ripoti iliyopita.

Akiongea na Waandishi na wadau mbalimbali Jijin Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa (TPSF) Tanzania Private Sector Foundation Bw, Godfrey Simbeye amesema kuwa,Tanzania imeshika nafasi ya 137 kutoka nafasi ya 132 ya ripoti iliyopita na kutaja vipengele ambavyo imefanya vizuri kuwa ni, Utoaji wa mikopo, upande wa sheria na upatikanaji wa umeme.

Pia amezitaja sehemu ambazo Tanzania imefanya vibaya kuwa ni utoaji wa mizigo na uingizaji wa mizigo ya biashara, Tanzania imeshika nafasi ya 182 kati ya nchi 190 na kueleza serikali ya awamu hii inavyofanya mageuzi makubwa ili kuimarisha urahisi wa kufanya bishara nchini.

Kwa upande wa biashara za mipakani Mkurugenzi wa sera Bwn. Gilead Teri (TPSF) Tanzania Private Sector Foundation naye amesema kuwa, Tanzania imeshika nafasi ya 156 kati ya nchi 190 na kuelezea sababu zinazopelea changamoto katika eneo hilo la mipakani na jinsi ya kuzitatua.

Amesema kuwa changamoto za muda na gharama ambazo wawekezaji hutumia mipakani kufanya biashara ni moja ya changamoto inayozingatiwa.

Pia amesema kufunguliwa kwa kituo cha pamoja mtukula na mengne yatafanya mwakan kuwa ripot nzuri kwa upande biashara za mpakani.

Aidha mkurugenzi mkuu Godfrey Sembeye ameeleza changamoto ya kutokuwepo kwa sheria ya kufanya biashara kwa mfumo wa kielectonic kama zinavyofanya nchi zilizoendelea kibiashara, kusain document mbalimbali bila kuonana yaan kupitia mfumo wa kimtandao kuwa n moja ya hatua zinazochukua muda.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*