​RC MNYETI ATIMIZA AHADI YAKE YA PIKIPIKI 26 KWA WATENDAJI  WA KATA HALMASHAURI YA MERU. 

Na Mwandishi Oscar Lyimo . 

Mkuu Wa Mkoa Wa Manyara Ndugu Alexander Mnyeti Jana Katika Ukumbi Wa Walemavu Uliopo Halmashauri Ya Meru Alikabidhi Takribani Pikipiki 26 Kwa Watendaji Wa Kata Zilizopo Ndani Ya Meru Ahadi Aliyotoa Akiwa Mkuu Wa Wilaya Hiyo. 

Rc Mnyeti Akikabidhi Pikipiki Hizo Kwa Watendaji Wa Kata Alisisitiza Juu Ya Uchapakazi Kwa Watumishi Hao Kwani Hawana Sababu Tena Ya Kutowatumikia Wananchi Kwa Weledi Mkubwa Kwani Serikali Imewapatia Vitendea Kazi Hivyo Usafiri Ili Kuleta Ufanisi Wa Kazi Mintarafu Rc Mnyeti Aliendelea Kutoa Semina Elekezi Kwa Watumishi Wengine Waliohudhuria Ugawaji Wa Pikipiki Hizo Kwa Kuweka Mkazo Juu Ya Uwajibikaji, Nidhamu, Na Utendaji Mzuri Kwa Serikali Na Atayechukua Nafasi Yake Ya Ukuu Wa Wilaya Ya Arumeru. 

Mosi Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Meru Ndugu Christopher Kazeri Akizungumza Pia Na Watendaji Hao Alisema Anamshukuru Sana Rc Mnyeti Katika Kipindi Chote Alichokaa Arumeru Kwa Kuwa Mbunifu(creative) Katika Masuala Mbalimbali Ikiwemo Upatikanaji Wa Pikipiki Hizo Kwa Watendaji Wa Kata Na Amemuomba Pia Asishite Kuja Kutoa Ushirikiano Huo Huo Atakapomuitaji Kwani Hii Bado Ni Halmashauri Yake, Mathalani Ndugu Kazeri Alitoa Wito Kwa Watumishi Wengine Kufanya Kazi Kwa Bidii Sana Kama Rc Mnyeti Ndio Maana Rais John Pombe Magufuli Akaona Anafaa Kuvaa Viatu Vya Ukuu Wa Mkoa Wa Manyara. 

Naye Katibu Tawala Wa Halmashauri Ya Meru Ndugu Mzava Alitoa Pongezi Zake Za Dhati Sana Kwa Rc Mnyeti Kwanza Kwa Kuteuliwa Kuwa Mkuu Wa Mkoa Wa Manyara Na Kuja Kutimiza Ahadi Yake Ya Pikipiki Kwa Watendaji Wa Kata Kipindi Alipokuwa Mkuu Wa Wilaya Hii Na Kwamba Rc Mnyeti Amekuwa Mwalimu Wake Mkubwa Sana Kwenye Masuala Mengi Ya Utumishi Ukiachilia Pia Maisha Nje Ya Kazi Na Kwamba Anastahili Nafasi Hiyo Ya Ukuu Wa Mkoa Kwa Kazi Nzuri Aliyofanya Hapa Arumeru Ukiachilia Utoaji Wa Pikipiki. DAS Mzava Alisisitiza Pia Hakika Manyara Imepata Jembe La Kazi Na Watumishi Wa Mkoa Wa Manyara Wampe Ushirikiano Wa Kutosha Kama Arumeru Walivyompa Na Anamtakia Heri Na Fanaka Kwenye Nafasi Yake Mpya Ya Ukuu Wa Mkoa. 

Mosi Diwani Lengai Ole Saba Wa Kata Ya Sambasha Aliyekuwa Pia Mwenyekiti Wa Uvccm Mkoa Wa Arusha Akizungumza Kwa Niaba Ya Madiwani Wa Arumeru Alitoa Pongezi Nyingi Sana Kwa Rc Mnyeti Kwa Kuteuliwa Kwake Kuwa Mkuu Wa Mkoa Wa Manyara Na Kwamba Utukufu Wa Nyumba Ya Mwisho Umekuwa Mkubwa Kuliko Wa Mwanzo Na Hiyo Ni Onyo Kwa Wale Wote Wenye Nia Ovu Juu Ya Utendaji Wa Rc Mnyeti Kuwa Wapo Watu Wanaona Huko Nje Uchapakazi Wake Mintarafu Yeye Na Madiwani Wenzake Wamefurahi Sana Kwa Kitendo Chake Cha Utoaji Wa Pikipiki 26 Kwa Watendaji Wa Kata Zote Zilizopo Ndani Ya Meru Utakuza Ufanisi Mkubwa Kwa Watendaji Hao Kwani Wamekuwa Wakiona Changamoto Wanazopitia Kwenye Kutimiza Majukumu Yao Kwa Wananchi. Mathalani Diwani Sabaya Amesema Wale Wote Wanaosema Ccm Imepoteza Muelekeo Kwamba Wao Ndio Wamepoteza Uelekeo Kwa Kufisidi Nchi Hii Kwa Kuuza Wanyama Wetu Wa Hifadhi Kama Twiga Nje Ya Nchi Na Kwa Sasa Ccm Ndio Inazidi Kuimarika Zaidi Kwa Kupata Viongozi Kama Rc Mnyeti Wanaotekeleza Ilani Ya Ccm Kwa Vitendo Zaidi. 

Akipokea Pikipiki Hizo Mtendaji Mbise Alisema Kwa Niaba Ya Watendaji Wote Wa Kata 26 Wanamshukuru Sana Aliyekuwa Mkuu Wa Wilaya Ndugu Mnyeti Ambaye Kwa Sasa Ni Mkuu Wa Mkoa Wa Manyara Kwa Kutimiza Ahadi Yake Hiyo Ya Pikipiki Ambazo Zitaleta Ufanisi Mkubwa Kwao Katika Kuwatumikia Wananchi Wa Meru Kwa Mawanda Mapana Hivyo Watamuunga Mkono Rais Magufuli Kwa Kufanya Kazi Kwa Vitendo Zaidi Na Weledi Ili Kujenga Tanzania Mpya Yenye Falsafa Ya “Hapa Kazi Tu” Kwa Kumuombea Mungu Amtangulie Huko Aendako Katika Majukumu Yake Mapya Na Watamkumbuka Kwa Mengi Mazuri Sana Aliyofanya Ndani Ya Halmashauri Hiyo Kama Utatuzi Wa Migogoro Ya Ardhi Ambayo Imekishwa Kabisa Katika Kata Zao, Suala La Changamoto Maji Kupungua Sana Kwenye Kata Zao, Uboreshaji Wa Miundombinu Hususani Barabara Nyingi Zinapitika Kwa Sasa, Vifaa Tiba Na Madawa Kwenye Hospitali Zetu Na Vituo Vya Afya Kuongezeka, Njia Za Mawasiliano Kuboreshwa, Shule Za Sekondari Na Msingi Kuboreshwa Kwa Upande Wa Vitendea Kazi Kama Vifaa Vya Maabara, Vitabu Vya Kujifunzia Na Kusomea N.k, Mtendaji Mbise Alisema Yapo Mengi Sana Ya Ubunifu Mkubwa Aliyofanya Rc Mnyeti Kwa Arumeru Kubwa Sana Watakalomkumbuka Pia Ni Kutokomeza Madawa Ya Kulevya Hususani Bangi Ambayo Imewathiri Vijana Wengi Ambao Ndio Nguvu Kazi Kwa Taifa Ambapo Sasa Bangi Hiyo Imetoweka Kwa Kiwango Kikubwa Sana Tofauti Na Huko Nyuma. 

Akihitimisha Kwenye Hotuba Yake Rc Mnyeti Alitoa Pongezi Nyingi Sana Kwa Viongozi Wa Ccm Kwa Utekelezaji Wa Ilani Kwa Vitendo, Viongozi Wa Asasi Mbalimbali Kwa Ushirikiano Mzuri Toka Kwao Alipokuwa Mkuu Wa Wilaya Hiyo, Wafanyakazi Wa Halmashauri Zote Mbili Meru Na Arusha Dc, Watumishi Wote Kwa Nafasi Zao Mbalimbali Ambao Walikuwa Naye Bega Kwa Bega Katika Utumishi Wake Kwa Wananchi Na Kuwaomba Wamuunge Mkono Mkuu Wa Wilaya Anayekaimu Kwa Sasa Ndugu David Chorongo Ili Kuwe Na Uwajibikaji Wa Pamoja (Collectively Responsibility) Katika Utendaji Wao. 

Rc Mnyeti Pia Amevishukuru Sana Vyombo Vyote Vya Usalama Kwa Kumpa Ushirikiano Kuntu Kwa Kipindi Chote Cha Mwaka Mmoja Na Robo Cha Kuwatumikia Wananchi Wa Arumeru Na Kuviomba Viendelee Na Moyo Huo Huo Kwa Atakayechukua Nafasi Yake Ya Ukuu Wa Wilaya Kwa Kumsaidia Pia Kulinda Usalama Wa Raia Na Mali Zao. Pongezi Nyingi Pia Alitoa Kwa Wasaidizi Wake Na Madiwani Waliomuunga Mkono Katika Utatuzi Wa Changamoto Za Wananchi Wao Na Kuwapa Nasaha Kuendeleza Uzalendo Huo Kwa Wananchi Na Taifa. 

Napenda Kuambatanisha Picha Za Matukio Mbalimbali Ya Ugawaji Wa Pikipiki Uliofanywa Na Rc Mnyeti Kwa Kutimiza Ahadi Yake Kwa Halmashauri Ya Meru. 

Wasalamu. 

Na Mwandishi. 
Oscar Lyimo. 
Arumeru.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*