​MAVUNDE,LUSINDE NA KUNAMBI WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI NA KUELEZEA MIKAKATI YA DODOMA MPYA.


Mbunge wa Jimbo la Mtera Mh Livingstone Lusinde na Mbunge wa 

Dodoma Mjini  Anthony Mavunde wampongeza Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa uamuzi wake kuhamishia Makao makuu ya Serikali Dodoma na hivyo kuongeza fursa za kiuchumi katika mkoa wa Dodoma kupitia uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali zitakazotolewa.


Aidha wabunge hao wakizungumza leo katika kipindi cha 360 cha Clouds TV pia wamempongeza Mh Rais kwa uamuzi wake wa kuivunja CDA na kurudisha mamlaka ya utawala wa ardhi chini ya Manispaa ya Dodoma na kubadilisha mfumo wa umiliki ardhi kutoka katika upangaji(Lease Ground) kwenda kwenye mfumo wa hati ya umiliki.Ambapo kupitia mfumo huo Dodoma itapata fursa ya kuvutia zaidi wawekezaji wa muda mrefu tofauti ilivyokuwa awali.
Aidha Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Ndg Godwin Kunambi ameelezea mipango mikubwa ya ukuzaji mji wa Dodoma ikiwemo uharakishwaji wa huduma ya vibali vya ujenzi,upimaji wa maeneo na uboreshwa wa miundombinu na huduma za kijamii ili viende sambamba na ukuaji wa haraka wa mji wa Dodoma.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*