​MAMLAKA YA MAJI ARUSHA YASAINI MKATABA WA KUCHIMBA VISIMA 56


Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Arusha AUWSA imesaini mkataba wa uchimbaji visima 11 kati ya 56 vinavyotarajiwa kuchimbwa  kwaajili ya  jiji hilo katika hatua  ya Serikali kukabiliana na tatizo la ukosefu wa maji safi ambalo limekuwa changamoto katika jiji hilo.

 Kukamilika kwa visima hivyo kutawezesha wananchi wa jiji la Arusha kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa asili Mia 100.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha AUWSA Engineer Ruth Koya amesema mradi huo utakaogharimu kiasi cha fedha bilioni 476 ambao umelenga kuhakikisha jiji la Arusha linaondokana na tatizo la maji mara tu visima hivyo vitakapokamilika ili kuweza kuwapatia wananchi huduma hii muhimu.”Mhe. Waziri nakuahidi mradi huu nitahakikisha  nausimamia kwa makini na Weledi wa hali ya juu ili kuweza kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inavyokata na ilivyowaahidi wananchi kuwa itawapatia maji safi  na salama”amesema mkurugenzi huyo.

Aidha Engineer Ruth Koya ametaja maeneo ambayo yatachimbwa visima hivyo ni kama ifuatavyo ambapo kumekuwa na uhaba wa maji kwa mda mrefu sasa,Magereza(seed farm) vitachimbwa visima11,Valeska Mbugani vitachimbwa visima12,Maji moto vitachimbwa visima18,Tengeru Makumira Usariver vitachimbwa visima 15.

Akizungumza katika hafla hiyo ya waziri wa maji na umwagiliaji Mheshimiwa Mhandisi Isack Kamwelwe amemtaka mkandarasi kuhakikisha anamaliza kazi kwa wakati uliopangwa ili kuwatatulia kero za maji wananchi wa Arusha,Aidha waziri amesisitiza nia ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni kuhakikisha wananchi wake wanapata maji safi na salama hivyo amewataka watendaji wa sekta ya maji kufanya kazi kwa weledi na umakini ili kufikia lengo la serikali katika kuhakikisha maeneo yote nchini yameunganishwa kwenye huduma ya maji.

Akitoa shukrani kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Daqqaro ameishukuru serikali na AUWSA kwa hatua wanazochukua katika kutatua kero za wananchi kwenye sekta ya maji na kuahidi kufuatilia utekelezaji wa mradi huo kama ambavyo mkataba wake unasema.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*